Hauhitaji Motisha. Unahitaji Nidhamu Zaidi.

 


Leo, tutachunguza jinsi nidhamu inavyokuwa muhimu zaidi kuliko motisha katika kufikia mafanikio. Mara nyingi, watu wanatafuta motisha kuwafanya waanze jambo, lakini siri ya kudumisha mafanikio ni nidhamu. Hebu tuchimbue zaidi.

Motisha ni muhimu unapotaka kufanya jambo lolote na ni kweli inaweza kukuhamasisha kuanza safari yako ya mafanikio, au jambo lolote. Lakini kuwa na NIDHAMU pekee ndo kutakufanya uendelee na safari yako. Wengi hawatambui hili na mwishowe wanakata tamaa bila kujitahidi kuijenga NIDHAMU katika maisha yao.

1. Mafanikio Hayajali Hisia Zako

Ni kweli, mafanikio hayajali namna unavyohisi au kujisikia. Yanajali tu ikiwa utajitokeza kila siku kufanya kile ambacho inakupasa ukitimize katika wakati husika. Watu wengi wanadhani wanahitaji motisha, uhamasishaji au nishati ili kuanza kazi.

Ila uhalisia ni kwamba, mafanikio yanahitaji kujisemea POTELEA POTE, na kufanya ambacho kinahitajika.

2. Maisha yatakujaribu kwa mitihani isiyoisha

Kujenga nidhamu kunahitaji kujituma kila siku. Hata wakati mambo yanapokwenda kombo au unahisi kuchoka, nidhamu inakufanya uendelee na jitihada. Yani msamiati wa kukata tamaa inabidi uuondoe kabisa katika akili yako, na ujitume kila siku inayoenda kwa Mungu.

3. Kujiamini na Kusimamia Malengo

Nidhamu inakuhitaji uwe mwaminifu kwako mwenyewe. Jiwekee malengo na dhamira ya kuyatimiza bila kutegemea mtu mwingine. Ili kujenga nidhamu imara, ni muhimu kuwa mwaminifu kwa ratiba yako, malengo yako, na ahadi ulizojiwekea.

4. Uvutie Ujuzi na Uzoefu Kutoka kwa Wale Wanaofanya Vizuri

Ni kweli, marafiki wasio na nidhamu wanaweza kukuathiri. Unahitaji marafiki na uhusiano sahihi. Kuwa karibu na watu wenye malengo sawa na ambao wanakujenga. N katika zama hizi mitandao imetuoa nafasi ya kuungana na watu maarufu, wafanyabiashara waliofanikiwa zaidi duniani na kujifunza kutoka kwao kupitia videos, podcasts, vitabu, na makala zao.

5. Epuka vitu vinavyokidhi haja zako kwa muda mfupi

Jamii imetufundisha kufuatilia raha ya muda mfupi badala ya kusudi la maisha ya muda mrefu. Lakini jambo hili linapelekea tuwe wadhaifu. Kinachotokoea ni kwamba ubongo wetu unajibadilisha kwa kutaka raha za muda mfupi kila mara (instant gratification).

Kuwa hodari na imara kunatokana na kufuata lengo la maisha la muda mrefu.

Hitimisho: Kufikia mafanikio kunahitaji zaidi ya motisha. Inahitaji nidhamu. Kuwa na nidhamu kunamaanisha kujitolea kufanya kazi kila siku kuelekea malengo yako, hata wakati hisia zinapokuwa dhaifu. Usiruhusu vyanzo vingine kama burudani zisizo na msingi, umbea wa wasanii, kucheza games na kuangalia movie kulikopitiliza, vikuchukulie nguvu na nidhamu yako. Kuwa mwenye nguvu na imara katika kudhibiti mambo haya. Endelea kuwahamasisha na kuwaunganisha watu katika safari yako ya kujenga maisha yenye mafanikio.

Chapisha Maoni

0 Maoni