Huu ni mwendelezo wa chapisho la 48 Laws of Power ambalo ni utambulisho wa makala mfululizo kuhusu kitabu hiki ambacho ni maarufu sana duniani kote kuhusu sheria za kupata nguvu na mamlaka. Kila makala ya muendelezo itahusisha walau sheria tatu (03) katika sheria 48 zilizo kwenye kitabu hiki.
Karibu MAISHA MAX ambapo kuna mengi ya kujifunza na kukuwezesha kupata MAARIFA, kuimarisha AFYA pamoja na kujiwezesha kwenye sekta ya UCHUMI. Pia tunapatikana katika mitandao ya kijamii; X 'twitter', Facebook, Tiktok, Youtube, Instagram, Telegram.
Sheria ya 1: Never Outshine the Master (Using'are sana kuzidi mkubwa wako).
- Jitahidi kumfanya Mkubwa wako aonekane mzuri kwa maana kutamsaidia yeye aonekane ni mwenye ufanisi kutokana na juhudi zako, hivyo utajizolea sifa zaidi kwake.
- Ni muhimu kuwa makini na jinsi unavyofanya hivyo, jitahidi kufanya harakati zako kwa usiri kiasi, kwani wenzako ambao mpo nafasi sawa wanaweza kuona unataka kuwaharibia kwa kutaka wewe ndo uonekane muda wote na wakakuletea kiburi.
- Uliza mara kwa mara ushauri na elimu juu ya mambo mbalimbali ambayo mkubwa wako anayafahamu.
- Pia yahusianishe mawazo yako mazuri na mwongozo ambao amekupatia mkubwa wako.
- Kama wewe ni noma sana, kuna wakati huna budi kujifanya hamnazo.
- Hata kama Mkubwa wako anakukubali, usijisahau sana. Kibao kinaweza kukugeukia muda wowote.
- Mpe Mkubwa wako hadhi
- Jitahidi kumfanya Mkubwa wako aonekane mzuri kwa maana kutamsaidia yeye aonekane ni mwenye ufanisi kutokana na juhudi zako, hivyo utajizolea sifa zaidi kwake.
- Ni muhimu kuwa makini na jinsi unavyofanya hivyo, jitahidi kufanya harakati zako kwa usiri kiasi, kwani wenzako ambao mpo nafasi sawa wanaweza kuona unataka kuwaharibia kwa kutaka wewe ndo uonekane muda wote na wakakuletea kiburi.
- Uliza mara kwa mara ushauri na elimu juu ya mambo mbalimbali ambayo mkubwa wako anayafahamu.
- Pia yahusianishe mawazo yako mazuri na mwongozo ambao amekupatia mkubwa wako.
- Epuka kujionyesha kuwa bora zaidi kuliko Mkubwa wako.
- Kama wewe ni noma sana, kuna wakati huna budi kujifanya hamnazo.
- Hata kama Mkubwa wako anakukubali, usijisahau sana. Kibao kinaweza kukugeukia muda wowote.
Kinyume cha Sheria hii;
- Ikiwa Mkubwa wako anaanza kupoteza nguvu au mamlaka, unaweza kufikiria kuvunja sheria hii. Katika mazingira hayo, inaweza kuwa na faida zaidi kuchagiza kasi ya upotezaji wa mamlaka yake, ili upate nafasi ya kung'ara wewe.
Sheria ya 2: Never put too much trust in friends, learn how to use enemies (Usiweke imani kubwa sana kwenye marafiki, jifunze namna ya kutumia adui zako).
- Kuna uwezekano mkubwa kuwa hauwafahamu marafiki zako kama unavyodhani, mara nyingi marafiki wataficha ukweli ili kuepuka malumbano.
- Kuchanganya urafiki na kazi kunaweza kuleta shida.
- Pia kumpa kazi au kumuajiri rafiki yako, kunaweza kuleta shida kwa sababu rafiki yako anaweza akachukizwa na ile hisia ya kujua inabidi akunufaishe au anaweza kutamani upendeleo fulani kutoka kwako.
- Adui zako wanaweza kuwa na manufaa kwako.
- Adui anaweza kuwa na faida kuliko rafiki, sababu ana kiu ya kuonyesha ubora wake na hatarajii upendeleo kutoka kwako.
- Adui ambao watabaki na uadui wao dhidi yako, pia wana manufaa kwa maana unaweza kuwatumia pia, kila story ina shujaa na adui.
Kwenye sheria hii, kuna mfano wa Mfamle Michael III wa Falme ya Byzantine ambaye alimuamini rafiki yake Basilius. Basilius alikuwa ni mfanyakazi kwenye zizi la farasi na kuna wakati aliokoa maisha ya Michael baada ya farasi mmoja kukata kamba na kupatwa na ukichaa. Kama shukrani, Michael alimpatia zawadi nyingi na akampatia nafasi ya mshauri wake wa kuaminika. Mwisho, Basilius alijilimbikizia mali nyingi na madaraka, alikataa kumrudishia Michael pesa zake, na mwisho alishiriki kwenye njama na kumuua Michael.
Kinyume cha Sheria hii;
Kuna wakati rafiki anaweza kuwa na manufaa zaidi kuliko adui. Anachoshauri Greene ni kumtumia rafiki yako kufanya kazi zako chafu au kumtumia kama mbuzi wa kafara endapo utabananishwa. Hii inafanya kazi vizuri sana kwa sababu ni rahisi watu kuamini ukweli kwamba mpaka imefikia hatua umemtoa kafara rafiki yako basi ni kweli amekosea na wewe huna makosa.
Sheria ya 3: Conceal your intentions (Kuwa na usiri mkubwa juu ya nia zako).
- Watu wengi huweka mambo yao wazi, hutoa mawazo na hisia zao kwa urahisi sana, na wana imani kwamba ukweli ndo utawasaidia kuziteka nyoyo za wengine. Mtazamo wa Greene ni tofauti, hoja yake ni kwamba tabia hii ni kama stori za Abunuwasi. Uhalisia ni kwamba ukweli huwachukiza watu wengi.
- Usiweke mambo yako wazi.
- Kuwashirikisha wengine juu ya mawazo yako kutakufanya uonekane ni rafiki na mwaminifu mbele ya macho yao, hasa kwenye stori zako ukiweka namna wewe ni “muumini wa ukweli”.
- Kuigiza kama unakubaliana na watu, ilihali haukubaliani nao kunakuongezea nguvu wewe.
- Matumizi ya chambo na mapazia ya moshi yatawapa adui zako ugumu wa kupanga njama dhidi yako, lakini pia ugumu kwenye kupangua mashambulizi yako.
- Tengeneza hali flani ya usiri, ukifunguka sana utazoeleka kiurahisi, na mwisho utakosa heshima na watu watakudharau.
Ukiwa unajaribu kumvuta mtu, ya kung’ata na kupuliza ndo inaleta utamu zaidi. Watu wanapenda kudanganywa kuliko uhalisia wa mambo ulivyo na ndio maana wanasiasa ni wataalamu sana kwenye kudanganya. Ila mtu akifahamu kwamba unang’ata na kupuliza, ni rahisi kukuchukia.
Kinyume cha sheria hii;
Ukijifanya kama mjinga na watu wanakujua wewe ni chatu, watu watakuona umejaa unafiki uliopitiliza. Kama upo kwenye kundi hilo ni vyema kuendelea na tabia yako huku ukijaribu kutafuta toba kwa ujanja.
Tutaendelea na uchambuzi wa kitabu hiki cha 48 Laws of Power kwenye makala zinazoendelea, KAA MKAO WA KULA.
0 Maoni