NJIA YA KUPUNGUZA UZITO #1 - LISHE


VIDEO YA YOUTUBE KUHUSU VYAKULA

Maboresho makubwa zaidi unayoweza kuyafanya kwa ajili ya afya yako na maisha yako kiujumla ni kupunguza uzito wa ziada.

Kuwa mnene ni jambo gumu, japo watu wanaweza kukuita "cute" na "healthy" wanapomaanisha "kibonge" ni unafiki.

Kuwa na uzito wa ziada, kubali au kataa, inapunguza fursa za kazi, inaharibu sifa yako, hupunguza kujiamini na pia heshima yako mwenyewe, kuharibu magoti yako, kuharibu mwili wako mzima, mifumo yake yote na viungo vyake; na kuharibu udhibiti wa homoni. Hata hivyo, tayari unajua hilo ndio maana unasoma ukurasa huu.

Binafsi sijawahi kuwa na uzito wa ziada, na nimekuwa na mwili wenye afya kwa muda mrefu. Napenda kuwa na mwili wenye afya zaidi na nina imani kila mtu anapenda hivyo.

Muhtasari mfupi kuhusu mada hii:

1. KULA VYAKULA VYA AFYA - VIDEO YA YOUTUBE KUHUSU VYAKULA 2. FANYA MAZOEZI Simple tu, ni hivyo.

Ila sasa twende kwa undani zaidi:

Chakula: Hii sehemu ni ngumu kwa watu wengi. Lakini usijali; nitakuongoza kupitia andiko hili ili ufahamu jinsi lishe yako inatakiwa kuwa ili kupunguza uzito.

VIDEO YA YOUTUBE KUHUSU VYAKULA

Inahusiana na kupunguza kiasi cha chakula unachokula (hakuna kitu kinachosaidia kupoteza uzito kama kula chakula kidogo) na kula vyakula vyenye kukujengea afya tu.

1. Kula milo michache: Fikiria kupunguza idadi ya milo yako kwa siku, hasa kifungua kinywa. Kula mara 2 badala ya 3 kwa siku (kawaida watu wengi hula mara 3) - hii itahakikisha unakula kalori chache siku nzima na itakusaidia kupoteza mafuta haraka.

2. Tafuna chakula chako vizuri: Watu wanene huwa hawatafuni chakula chao vya kutosha. Hawatambui wanachokula. Inachukua muda kwa ubongo kutambua kuwa tumbo limejaa, na kutafuna vizuri chakula kunafidia muda huo vizuri. Kutafuna kunahakikisha kiasi cha kutosha cha mate kinachanganywa na chakula. Hii inasaidia mmeng'enyo na unyonyaji wa virutubisho, hii inaendana na tafiti zilizofanyika kuhusu sayansi ya mmeng'enyo wa chakula. Ikiwa hautafuni chakula chako vizuri, mwili wako hautaweza kunyonya sehemu kubwa ya virutubisho.

3. Kula vyakula vya afya TU: Usile vyakula visivyokuwa na afya. Sio mara moja kwa siku, sio mara moja kwa wiki, sio mara moja kwa mwezi. Na pia usijiibie, mpaka ufikie lengo lako la uzito ambao utakupaka ustawi wa mwili. Ukijiibia unavunja ule msukumo wako. Mfano ukawa unakula pungufu ya kalori 200 kwa siku 6 mfulululizo halafu siku ya saba ukala kalori 1200, ni sawa na kufanya kazi bure yani umepoteza wiki nzima ya maboresho. Ongeza shauku yako ya kupunguza uzito. UNAWEZA KUFANYA. Watu wenye shauku dhaifu kuliko wewe wameweza, na pia watu wanene kuliko wewe wameweza. Jiamini kuwa unaweza.

Vyakula unavyopaswa kula:

  • Nyama
  • Samaki
  • Maziwa na bidhaa nyingine za maziwa (pamoja na siagi na jibini)
  • Mayai
  • Nafaka
  • Matunda
  • Mboga
  • Mchele
  • Viazi
  • Mafuta
  • Maji mengi
Vyakula vya kuepuka;
  • Vyakula vilivyosindikwa sana
  • Chips na bidhaa zingine zilizokaangwa sana
  • Bidhaa za "Low-Fat" na "Diet"
  • Mafuta ya mboga
  • Sukari
  • Vinywaji laini
  • Viongezeo bandia vya utamu
  • Biskuti
  • Margarine (Siagi bandia)
  • Ikiwa wewe ni mwanaume: Kitu chochote kilichotengenezwa kutoka kwa soya

4. Tumia sahani ndogo wakati wa kula: Utafiti umeonyesha kuwa kubadilisha sahani ndogo kimakusudi hufanya watu kula sehemu ndogo na kuokoa kalori nyingi zaidi.

5. Punguza kalori kwa kuepuka vinywaji: Vinywaji laini, na vinywaji vingine vimejaa sukari (au mbaya zaidi: syrup ya nafaka ya juu) na havijazai tumbo lako. Hasa pombe. Usiipe figo yako mzigo mkubwa. Ni rahisi sana kuingiza kalori 250 mwilini kwa dakika chache kwa vinywaji ambavyo havikukidhi hata kidogo. Kinywaji pekee unachopaswa kunywa ni maji, ambapo tunakuja kwenye point inayofuata...

6. Kunywa lita 4 - 6 za maji: Maji ni kinywaji kamili cha kukukidhi, yana kalori sifuri na yanakidhi tumbo lako. Watu wengi hawanywi maji ya kutosha. Napendekeza kuweka chupa ya maji karibu na kitanda chako na kunywa glasi mara moja mapema asubuhi tu unapoamka.

7. Lala saa 8 kwa siku: Watu wengi hulala klwa muda kidogo. Kupata usingizi wa kutosha kutakusaidia kurekebisha mzunguko wako wa kimetaboliki na homoni zako. Hii italeta miujiza kwa afya yako na misuli yako, na kukusaidia kupoteza mafuta.

8. Kula vyakula VYENYE PROTINI. nyingi: Hii ni muhimu sana sana sana. Unapaswa kula vyakula VYENYE PROTINI. nyingi. Vyakula hivi vitakusaidia

  • Kukushibisha haraka na kukufanya uhisi umekinai na hivyo kupunguza njaa.
  •  Kupunguza mafuta mwilini, na kukusaidia kuwa na uzani wa kawaida.
  • 9. Jijengee tabia ya kunywa kahawa: Inaongeza uwezo wako wa kimetaboliki. Inaupa mwili wako nishati. Nina imani hii haihitaji maelezo zaidi.

    10. Pumua vizuri: Choma mafuta yako kwa pumzi yako. Pumua kwa kina na kwa tumbo lako. Hii ni hekima ya kale. Inaboresha uwezo wako wa kimetaboliki na kukupatia utulivu.

    Makala hii imeendelea katika sehemu ya 2 - Mazoezi

    Chapisha Maoni

    0 Maoni