Kujuta ni hisia isiyofaa


Kuna theory katika uchumi inaitwa "sunk cost fallacy" / "dhana ya gharama iliyozama"

"Katika uchumi na maamuzi ya biashara, gharama iliyozama ni ile ambayo tayari imetumika na haiwezi kurejeshwa."

Hii pia inatumika katika maisha.

Umewahi kuona mtu akisikitika na kuwa na huzuni kubwa kuhusu jambo baya lililotokea hapo awali (kawaida muda mrefu uliopita)? Najua umewahi.

Binafsi nasema hupaswi kuwa hivyo.

Kusikitika ni kupoteza muda na kujuta ni hisia isiyofaa.

Ni upotezaji kamili.

Yaliyopita tayari yamekwisha. Gharama imeshatumika. Haiwezi kurejeshwa.

(Ikiwa inaweza kurekebishwa, basi usipoteze muda kusikitika; endelea na kufanya hivyo.)

Labda ulifanya kosa. Labda ulifanya uamuzi mbaya, lakini hiyo imeshatokea.

Huna njia ya kufuta hilo.

Kitu pekee unachopata kwa kuzingatia sana siku zako za nyuma ni huzuni, shaka kuhusu nafsi yako, na hali ya kujisikia vibaya.

Ni kweli, inakupasa kurekebisha kile unachoweza kurekebisha kwenye kilichotokea, lakini kile ambacho huwezi kurekebisha ni lazima ukubali kama kilivyo. Kufanya hivi ni ufunguo muhimu wa kukupatia furaha.

Niruhusu nikupe na mfano:

Tufanye nakupa milioni 1 TZs. Siku ya kwanza, ukapoteza laki 5.

Siku ya pili, unasikitika kwamba mwanzo ulikuwa na 1M halafu sahivi una laki 5 . Hilo ni wazo lisilofaa. Kwa nini sasa ujiweke katika majonzi ?

Siku ya pili, wewe ni mtu mwenye laki 5 tu, sio mtu ambaye amepoteza laki 5 jana. Hii ni kwa sababu hio ndio hali yako ya SASA. Unatakiwa kujali kuhusu hiyo.

Unaweza kufanya maamuzi mazuri kulingana na namna gani rasilimali zako za sasa zinaweza kuathiri mustakabali wako, sio jinsi rasilimali zako za zamani zinavyoweza kufanya hivyo.

Kwa hiyo, siku zako za nyuma hazifai kuziwekea majuto, zichukulie kama mafunzo.

Chapisha Maoni

0 Maoni