Hii makala inaendelea kutoka Sehemu #2: Mazoezi.
Tayari nimezungumzia kuhusu kupoteza mafuta kwa kutumia lishe na mazoezi.
Tuanze na ukweli kwamba kwenye maisha yako kitu ambacho uko nacho muda wote wa uhai wako ni mwili wako mwenyewe. Je, kuna tabia unapaswa kuwa nazo ili kuitunza hii mali yako pekee ?
Jibu ni dhahiri, itunze, itunze vizuri, ihifadhi iwe na afya na nguvu kadri unavyoweza.
Kama umefuatilia vizuri kwenye makala yangu nimegusia mikakati ya muda mrefu.
Nimependekeza suluhisho za muda mrefu kwa mazoezi na lishe.
Hiyo ni kwa sababu kupunguza mafuta na kuwa fit ni mabadiliko ya mtindo wa maisha kwa ujumla. Sio jambo la mara moja. Lazima uendelee kuwa fiti.
Kuna mzunguko huu wa kichocheo -hatua - thawabu (cue - action - reward) ambao unaendesha tabia na maisha yetu, kama una changamoto ya kiafya inawezekana mzunguko huu haupo sawa.
Unataka chakula zaidi kwa sababu wewe ni mnene, na wewe ni mnene kwa sababu unataka chakula zaidi. Ni kitendawili.
Lakini ukijipa muda, hilo litabadilika utavunja mzunguko huu na mambo yatakuwa bora.
Inahitaji kazi, lakini nawaahidi kuwa inakuwa rahisi baada ya muda na azma yako ya dhati ya kufikia malengo ya kiafya unayohitaji.
Wiki 4: Unanza kugundua mabadiliko ndani ya mwili wako.
Wiki 8: Marafiki na familia wananza kuona mabadiliko ndani yako.
Wiki 12: Kila mtu anaweza kuona kuwa mwili wako unabadilika kuwa bora kama unavyohitaji.
Unapaswa kuendelea, inavutia sana kuona matokeo. Jiwekee tu wiki 4, mabadiliko katika lishe na kuanza mazoezi ya asubuhi yataleta tofauti ambayo utajivunia nayo.
Katika mwezi wa pili ukiongeza mazoezi mengine ya misuli, utazidi kuona mabadiliko chanya katika mwili pamoja na nafsi.
Baadhi ya vidokezo kufanya safari yako iwe ya kufurahisha zaidi:
- 1. Usinunue vyakula vya hovyo: Mapambano halisi huanzia dukani, kila mtu inabidi ale na kuna ushauri na vyanzo mbalimbali ambavyo vimezungumzia vyakula vyenye kujenga mwili wako vizuri. Kama huna kwenye friji lako, huwezi kula unapojisikia njaa ghafla.
- 2. Weka chakula chenye afya karibu nawe: Weka tunda au ndizi au mayai yaliyochemshwa chumbani mwako - unaweza kula unapojisikia njaa (au kuchoka).
- 3. Ikibidi badili marafiki zako: Unakwenda kula na marafiki zako wanaagiza pizza na jibini zaidi - wewe unakata kitunguu na pizza nyembamba. Angalau sio mbaya kama wanavyokula. Na hivi karibuni, unagundua umeanza kuongeza unene kuzunguka tumbo lako. Usiwe karibu sana na watu wanene. Inajulikana kuwa kuwa na marafiki wanene kunakufanya kuwa mnene - kwa sababu marafiki zako wanavyoathiri tabia zako. Boresha mduara wako wa kijamii. Hii inaweza kuwa ngumu kidogo, haswa ikiwa unafanya kazi na watu wanene. Itakuwa mabadiliko makubwa utakayofanya kwa muda mfupi - na mabadiliko mazuri sana.
Ndiyo na Hapana, tuseme hauhitaji kufanya chochote, unaweza kuendelea kulala tu kwenye sofa na kucheki TV siku nzima, na hatua kwa hatua uupate unene tena. Au, unaweza kuendelea na kazi - PIGA HATUA MBELE boresha maisha yako milele, hakuna wa kukusaidia kwenye hili.
Kumbuka, fitness ni mtindo wa maisha, sio tukio flani katika maisha yako.
Itaanza kuwa rahisi mara tu unapoona matokeo, hautauliza swali hili tena. Utataka kuendelea kufanya hivyo.
Tafadhali jifanyie jambo hili jema: tenga wiki 4. Hautajutia. Hakuna visingizio wala kulalamika - do the work.
0 Maoni