Kama ulikuwa unajiuliza utatokaje kwenye mtego huu, basi leo ninakuletea trick ambazo watu wanaweza kuzitumia kwenye mazungumzo na wewe, lakini pia nitakujulisha namna ya kuzipangua hila zao na ukalinda heshima yako ambayo kama hautakuwa makini utaishusha endapo utakurupuka.
Ila kitu cha msingi zaidi kwenye kujinasua kutoka kwenye mtego huu, ni kwanza kuelewa nini kinaendelea kabla haujachelewa. Kikawaida, mtu ambaye ana njama hizi utamuona mwanzoni kabisa mwa mazungumzo kwa kutumia sauti ya ukali kidogo, au kutumia maneno ambayo unaona kabisa amelenga kukushambulia.
Ninayasema haya kwa kuwa kuna wakati nilipata nafasi ya kuwa kwenye nafasi ya uongozi, ambayo ilikuwa imegubikwa na misukosuko kwa maana kulikuwa na hila za kutaka kuotesha nyasi kwenye kibarua changu kidogo sana.
Post hii iko na muundo wa point husika pamoja na mifano, lengo langu ni kuonyesha namna nzuri ya kuendesha majibizano na kushinda, nina imani utafurahia pamoja na kujifunza
1. Kitu cha kwanza, usimjibu mtu hoja yake kwa kudakia.
Muache amalize anachotaka kusema, ziweke hisia pembeni kwanza na kuwa kama simba aliyetulia kabla ya kumnyakua swala ambaye tayari yupo kwenye 18 zake.
Lakini sambamba na hilo, usijibu hoja ya mtu, kabla haujaitafakari na kutengeneza summary ambayo unahisi atavutiwa nayo,
Hii inahusisha kauli kama, kwahiyo unasema desh desh desh, usiharakie kutafuta majibu ambayo hayatakufanikishia lengo la kushinda mabishano hayo.
Hapa, unamuonyesha mtu unayezungumza naye kwamba umesikiliza alichosema kwa ukaribu na umakini mkubwa sana.
Onyesha kwamba wanachokisema kinafaa kukipa umakini wako, ni asili ya binadamu kupenda attention.
Kwahiyo kwa lugha rahisi hapa unarudisha maneno yao kwamba nimekuelewa ulichomaanisha na ni hiki hapa.
2. Kuwa mwepesi kujua watu wanapobadilika kwenye maongezi ( Tuite hii “Hali ya kutaka kupigana Hahahah”)
Hii nimeisema awali, lakini kuna vielelezo ambavyo vipo wazi, vinaweza kukujulisha endapo mtu ameingia kwenye hali hii, ataongea kwa kubwatuka na hasira hadi kufikia hatua ya kuonyesha vidole, pamoja na kuingilia maongezi yako mara kwa mara.
Lakini pia kuna vielelezo ambavyo vimejificha na unaweza kuvibaini.
Mfano - Mwanzoni mwa maongezi, mtu akakwambia na kukuonyesha kwamba haamini MAWAZO uliyonayo huenda amesikia kutoka kwa wengine au laah, au tayari akawa na mtazamo wake kabla ya kukusikiliza, ujue tayari kuna shida.
3. Kama utaona hali hii jiandae kukwepa mitego ya kwenye mazungumzo.
Mojawapo ya mtego mkubwa kwenye mazungumzo, ni kukunukuu vibaya kwa makusudi. Hii inamuonyesha kana kwamba yeye ndo ameshika usukani wa mazungumzo, mtu anaweza akabadilisha ulichokisema kwa maneno machache tu na akabadilisha kabisa maana ya maneno yako kwa makusudi, na kama haupo makini ni ngumu kutambua. Mwisho utajaa katika 18 zake na atakudaka.
Unatakiwa kuwa makini kwa kutoruhusu mtu akunukuu vibaya, la sivyo utaishia kutetea mawazo ambayo yamepandikizwa kwenye kichwa chako.
Kuna trick moja ambayo unaweza kuitumia hapa kutegua huu mtego, omba nafasi ya kuyaimarisha mawazo pamoja na hoja zako kwa kuzisema, tena kwa ujasiri kabisa.
4. Usikubali kutolewa kwenye reli kwa kukatishwa mazungumzo.
Hii pia ni njia ambayo inatumika kwenye mazungumzo, unaongea mara ghafla mtu anaingilia kati, lengo hasa likiwa ni kukuyumbisha kabla haujafika kwenye hoja zako za msingi kabisa. Ni muhimu sana kuiepuka hali hii mana inaweza kukutoa mchezoni kweli kweli.
Lakini kitu cha kufanya hapa ni simple,
Kuna njia 3
Namba 1 - Tulia kwanza, msikilize point yake halafu endelea kuongea ulipoishia kwa utulivu hata kwa kumwambia anayeongea nimekuelewa vizuri kabisa.
Namba 2 - Tulia, chochote anachosema mtu kwa kuingilia kati, mwambie ninaheshimu sana mawazo na mtazamo wako ila binafsi ninafikiria ni hivi.
Namba 3 - Kabla ya kuongea hoja ya msingi, sema wazi kwamba hapa naomba usiniingilie wakati ninaongea, ila angalia isiwe umeingia kwenye “hali ya kutaka kupigana hahah” na ukiona ngoma ngumu sana tumia kidole cha shahada kama namna ya kuonyesha mamlaka, ila isiwe kama unamwambia yani WEWEEE NTAKUPIGA, laah iwe kama unaashiria kumwambia tuliaaa halafu uendelee kuongea, unaweza ukakichezesha pia maana kinaashiria mamlaka.
5. Kuwa makini kum’bamba anapokosa mantiki kwenye maongezi yake.
Lengo la mazungumzo/mabishano ni mtu mwingine kukushinda, na yupo tayari kutengeneza dhana za kusadikika ili tu akuoshee niseme. Hivyo inapasa kuwa makini ili kuzifichua stori na hoja ambazo hazina mantiki.
Mpaka kufikia hapa tumejadili namna za kujinasua na mtu ambaye anaonyesha kabisa hana nia nzuri na wewe kwenye mazungumzo, ila kuna mda majibizano yanaenda kwenye vitu ambavyo haupo tayari kuviongelea mfano kuongelea maisha yako binafsi mbele za watu.
Hii ikitokea una kila haki ya
6. Kuweka mipaka juu ya mambo ambayo haupo tayari kuyaweka wazi.
Kila mtu ana mambo ambayo hayupo tayari yawe wazi kwa watu wengine, ukikutana na hali hii inabidi uweke mipaka ila haimaanishi kwamba upayuke, unaweza tu kusema
Namba 1 - Sisjiskii kuongelea mada/hoja hii, hamna haja ya kuwa na uoga.
Okay, mpaka kufika hapa unajua namna ya kujinasua na mitego ya kimazungumzo/majibizano, lakini kuna jambo la muhimu bado sijaliongelea, nalo ni kurudisha hali ya utulivu kwenye hayo majibizano, na hii inatufikisha kwenye point no. 7
7. Kukiri kama kuna sehemu mawazo/hoja zenu zinafanana.
Hii ni njia nzuri ya kuondoa uhasama ambao inawezekana ulijengeka wakati majibizano yanaendelea, na kuleta ukaribu. Lakini unaweza kuingiza viashiria juu ya kutokubaliana kwenu katika hoja fulani, ila hii uifanye baada ya kukubali kwanza.
8. Jipe nafasi ya kubadilisha mtazamo wako.
Kwenye maongezi au majibizano yoyote, kuna wakati unaweza kufika na hoja zako zikawa hazina mashiko sana kiasi kwamba ukatamani kubadilisha mtazamo wako kwa kutumia mantiki
0 Maoni